Makala
Masharti Muhimu ya Visa ya Kutembelea Familia Saudi Arabia ya mwaka 2026.
Kuungana tena na familia yako nchini Saudi Arabia ni jambo muhimu kwa wengi wanaoishi na kufanya kazi huko. Ingawa Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia (MOFA) imerahisisha mfumo wa maombi ya visa, maelezo yote lazima yawe sahihi na nyaraka ziwe kamili. Kosa dogo linaweza kusababisha maombi kukataliwa.
Ili kupata Visa ya Kutembelea Familia (Family Visit Visa), mchakato unahusisha hatua mbili muhimu:
1: Masharti ya Mdhamini Aliye Saudi Arabia
Mwana Familia anayeishi Saudi Arabia ndiye anapaswa kuanzisha maombi kupitia tovuti rasmi ya huduma za visa ya MOFA. Atahitaji kuwa na:
Barua ya Mwaliko (Visa Invitation Letter) iliyotolewa na kuidhinishwa na MOFA.
Iqama na Pasipoti halali, zenye uhalali wa angalau siku 90.
Barua kutoka kwa mwajiri inayoonyesha mshahara na taaluma ya mdhamini, pamoja na uthibitisho unaohitajika kutoka Chama cha Biashara cha Saudi Arabia.
2: Masharti ya Waombaji Waliopo Nchini Kwao
Baada ya mwaliko kuidhinishwa, wana familia wanaoomba visa kutoka nje ya Saudi Arabia wanapaswa kuwasilisha nyaraka zao kwa ubalozi wa Saudi Arabia au kituo rasmi cha huduma za visa. Nyaraka hizo ni pamoja na:
Pasipoti halali yenye angalau miezi 6 kabla ya kuisha na kurasa mbili tupu.
Uthibitisho wa uhusiano wa kifamilia kama cheti cha ndoa kwa wanandoa au cheti cha kuzaliwa kwa watoto, kilichothibitishwa kulingana na taratibu zinazotakiwa.
Tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi pamoja na bima ya afya ya safari inayo kubalika na mfumo rasmi wa visa wa Saudi Arabia.
Hakikisha Maombi Yako Yako Sahihi
Hitilafu ndogo kama kuandika vibaya jina au namba ya pasipoti inaweza kusababisha mfumo kukataa maombi mara moja. Ndiyo maana ni muhimu kukagua nyaraka zote kwa makini kabla ya kuziwasilisha.
City Squares Inawezaje Kukusaidia?
City Squares inaweza kukusaidia:Kutafsiri na kukagua nyaraka za uhusiano wa kifamilia, Kuhakikisha taarifa za mdhamini na waombaji zinafanana, Kukuongoza katika hatua za uthibitishaji wa nyaraka, kukusaidia katika mchakato wa kuwakilisha maombi kwa ubalozi na vituo rasmi vya huduma za visa.
Wasiliana Nasi
Connect with us on WhatsApp ili kupanga mazungumzo na mshauri wetu.
Huduma Zetu
Usajili wa Kampuni Tanzania. Company Formation Service
Huduma zinazohusiana na Ubalozi wa Saudi Arabia.Saudi Embassy Services
Huduma za Ajira za Kimataifa. Employment Services
Huduma za Usafirishaji na Uondoaji wa Mizigo Forodhani. Logistics Services
Rasilimali Zaidi
Anzisha kampuni yako kupitia City Squares. Launch your business with City Squares
Weka miadi ya mazungumzo ya bure na mshauri wetu. Book a 1 on 1 Free Video Meeting with Our Expert Consultant
Jifunze zaidi kuhusu City Squares na huduma tunazotoa. Discover City Squares
Usafirishaji wa Makontena hadi Bandari ya Dar es Salaam
Kampuni Bora za Usafirishaji kutoka Ghuba hadi Tanzania
Je, Usafirishaji hadi Tanzania Unagharimu Kiasi Gani
Kampuni Bora ya Usafirishaji Tanzania
Taratibu za Forodha nchini Tanzania
Uko tayari kuanza mradi wako? Omba huduma yako na anza safari yako nasi!
Mtaalamu wa Kimataifa Mohammed bin Rashid bin Adwan