Makala

Kampuni za Uwekezaji (TIC) Tanzania: Jinsi ya Kupata Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji
2026-08-06 01:37:44
Wasiliana Nasi Sasa

Kampuni za Uwekezaji (TIC) Tanzania: Jinsi ya Kupata Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ni Nini?

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre – TIC) ni taasisi ya serikali inayohusika na kuhamasisha, kuratibu na kuwezesha uwekezaji katika Tanzania Bara.

Kilianzishwa chini ya Sheria ya Uwekezaji ya Tanzania, ambapo TIC hufanya kazi kama Kituo cha Huduma Mahali Pamoja (One-Stop Facilitation Centre) kinachowaunganisha wawekezaji wa ndani na wa kimataifa na taasisi mbalimbali za serikali.

Kupata Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji (Certificate of Incentives) kunawapa wawekezaji manufaa mbalimbali ya kifedha na yasiyo ya kifedha yanayosaidia kupunguza gharama za uwekezaji na kurahisisha uanzishaji wa biashara.

Kiwango cha Chini cha Mtaji Kinacho Hitajika

Ili mradi uweze kustahili kupata Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji, unatakiwa kufikia kiwango cha chini cha mtaji kulingana na aina ya umiliki wa biashara.


Wawekezaji wa Kigeni (Asilimia 100 au Ubia)

  • Kiwango cha chini cha uwekezaji ni Dola za Marekani 500,000 (USD 500,000).

Wawekezaji wa Tanzania

  • Kiwango cha chini cha uwekezaji ni Dola za Marekani 50,000 (USD 50,000).

Wawekezaji wa Kimkakati (Strategic Investors)

  • Miradi yenye thamani ya kuanzia Dola za Marekani Milioni 50 (USD 50,000,000) au zaidi.

Faida za Kupata Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji

  1. Vivutio vya kodi (Fiscal Incentives)

  • Msamaha wa Ushuru wa Forodha. Wawekezaji wanaweza kupata viwango maalumu vya ushuru au misamaha kwa uagizaji wa, Mitambo,Mashine na Vifaa vya uzalishaji Mali nyingine za mtaji zinazotumika katika utekelezaji wa mradi.


  •  Ahueni ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT); Wawekezaji wanaweza kunufaika na utaratibu maalumu wa kuahirisha malipo ya VAT kwa baadhi ya mali za mtaji zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.

  • Makato ya Mtaji kwa Asilimia 100; Sheria za kodi zinaweza kuruhusu makato ya haraka kwa matumizi yaliyofanywa katika: Majengo ya viwanda, Mitambo, Mashine, Mali nyingine za uzalishaji zinazo stahili.

2. Vivutio Visivyo vya Kikodi (Non-Fiscal Incentives)

  • Vibali vya Kazi kwa Wataalamu wa Kigeni; Wawekezaji wanaweza kuomba hadi vibali vitano (5) vya kazi na ukaazi kwa watumishi muhimu wa kigeni, kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazotumika.

  • Uhuru wa Kuhamisha Mtaji na Faida; Wawekezaji wanaruhusiwa kuhamisha, Faida halali za biashara, Gawio kwa wanahisa, Malipo ya mikopo ya kigeni ,kupitia benki zilizoidhinishwa nchini Tanzania, kwa mujibu wa sheria za fedha za kigeni.

  • Upatikanaji wa Ardhi kwa Uwekezaji; TIC hutoa msaada kwa wawekezaji katika kupata haki za matumizi ya ardhi kwa muda mrefu kupitia Benki ya Ardhi ya TIC kwa miradi inayostahili.

Mahitaji ya Kuomba Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji

Wawekezaji wanatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

  1. Mpango wa Biashara (Business Plan) au Upembuzi Yakinifu (Feasibility Study) inayoonyesha: Gharama za uwekezaji, Makadirio ya mapato na matumizi, Fursa za ajira zitakazo zalishwa.

  2. Nakala iliyothibitishwa ya: Cheti cha Usajili wa Kampuni (Certificate of Incorporation), Memorandum and Articles of Association (MemArts).

  3. Uthibitisho wa umiliki au matumizi ya ardhi, kama vile: Hati ya Ardhi (Title Deed), Mkataba wa Pango (Lease Agreement),Barua ya Ugawaji wa Ardhi.

  4. Fomu za maombi za TIC zilizojazwa kikamilifu pamoja na ada za serikali zinazotakiwa kwa ajili ya maombi na utoaji wa cheti.

Faida ya Kituo cha Huduma Mahali Pamoja cha TIC

Kupitia One-Stop Facilitation Centre, wawekezaji wanaweza kupata huduma kutoka taasisi mbalimbali za serikali katika eneo moja, iki wemo:

  • Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa usajili wa kodi.

  • Idara ya Uhamiaji na Wizara inayosimamia Kazi kwa vibali vya kazi na ukaazi.

  • Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa vibali vya mazingira.

  • BRELA, TBS, na OSHA kwa usajili na vibali vinavyohitajika katika shughuli za biashara.

City Squares Inawezaje Kukusaidia?

Kupata Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji kunahitaji maandalizi mazuri ya mpango wa biashara na uratibu mzuri na taasisi mbalimbali za serikali.

Kwa uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika ushauri wa uwekezaji na huduma kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa nchini Tanzania, City Squares inasimamia mchakato mzima wa usajili wa TIC kwa niaba yako.

Huduma zetu ni pamoja na:

  • Kuandaa Business Plan na Feasibility Study.

  • Kukamilisha maombi ya TIC.

  • Kuratibu mawasiliano na taasisi za serikali.

  • Kufuatilia upatikanaji wa Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji.

  • Kusaidia katika maombi ya vibali vya kazi na ukaazi kwa wawekezaji na wataalamu wa kigeni.

Tunarahisisha mchakato ili uweze kuanza na kuendeleza uwekezaji wako kwa ufanisi.

Wasiliana na City Squares

Je, unahitaji ushauri kuhusu uwekezaji nchini Tanzania au unataka kuomba Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji (TIC Certificate of Incentives)?

Wasiliana nasi kupitia Connect with us on WhatsApp, jaza fomu ya mawasiliano kwenye tovuti yetu,

 Au  Connect with us here panga kikao cha ana kwa ana au mtandaoni na mmoja wa wataalamu wetu wa uwekezaji.

Viungo vya Huduma Zetu

Rasilimali Muhimu

Machapisho ya Hivi Karibuni

06 Aug
Mwongozo wa Usajili wa Ubia na Biashara ya Mtu Binafsi Tanzania
Mwongozo wa Usajili wa Ubia na Biashara ya Mtu Binafsi Tanzania
06 Aug
Kampuni za Uwekezaji (TIC) Tanzania: Jinsi ya Kupata Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji
Kampuni za Uwekezaji (TIC) Tanzania: Jinsi ya Kupata Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji
06 Aug
Jinsi ya Kuanzisha Kampuni Binafsi Yenye Dhima Ndogo (Private Limited Company) Tanzania Mwaka 2026
Jinsi ya Kuanzisha Kampuni Binafsi Yenye Dhima Ndogo (Private Limited Company) Tanzania Mwaka 2026
06 Aug
Huduma za Usajili wa Kampuni Tanzania (Hatua Muhimu za Kufuata Mwaka 2026)
Huduma za Usajili wa Kampuni Tanzania (Hatua Muhimu za Kufuata Mwaka 2026)

Uko tayari kuanza mradi wako? Omba huduma yako na anza safari yako nasi!

Mtaalamu wa Kimataifa Mohammed bin Rashid bin Adwan

Mtaalamu wa Kimataifa Mohammed bin Rashid bin Adwan