Makala
Visa ya Umrah ya Mwaka Mmoja yenye Ingizo Nyingi: Masharti na Mwongozo wa Maombi
Wizara ya Hajj na Umrah ya Saudi Arabia inatoa Visa ya Umrah ya Mwaka Mmoja yenye Ingizo Nyingi (1-Year Multiple-Entry Umrah Visa). Visa hii ya digitali inamruhusu msafiri kuingia Saudi Arabia mara nyingi ndani ya kipindi cha siku 365 na kufanya Umrah mara kadhaa, huku akiwa na fursa ya kutembelea miji kama Makkah, Madinah, Jeddah na Riyadh.
Masharti Muhimu ya Visa ya Umrah yenye Ingizo Nyingi
Uhalali wa Siku 365: Visa hii huwa halali kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe ya kutolewa.
Kikomo cha Kukaa Siku 90: Mmiliki wa visa anaweza kukaa Saudi Arabia kwa jumla ya hadi siku 90 katika safari zote ndani ya kipindi cha visa. Siku hizi 90 hazianzi upya baada ya kutoka Saudi Arabia.
Mahitaji ya Huduma kupitia Nusuk: Kwa kila safari, mwombaji anatakiwa kuwa na huduma zilizo idhinishwa na kufanya booking pamoja na kupata kibali halali cha Umrah kupitia Nusuk App kabla ya kuwasili.
Kipindi cha Hajj: Visa hii haiwezi kutumika kuingia au kubaki Saudi Arabia wakati wa kipindi rasmi cha Hajj, kulingana na tarehe na masharti yaliyotolewa na mamlaka husika.
Hatua za Kuomba Visa ya Umrah
Hatua ya 1: Kupata BRN za Hoteli na Usafiri Zilizothibitishwa
Fanya booking ya malazi yaliyo idhinishwa na usafiri wa ndani ya Saudi Arabia ili kupata Booking Reference Numbers (BRNs) zinazotakiwa.
Hatua ya 2: Kukamilisha Mahitaji ya Afya na Chanjo
Pata chanjo ya lazima ya Meningococcal ACWY kutoka katika kituo cha afya kilichoidhinishwa na hakikisha una cheti cha chanjo.
Hatua ya 3: Kuwasilisha Nyaraka za Visa
Wasilisha pasipoti, picha, cheti/kadi ya chanjo na BRNs zinazohitajika kwa ajili ya mchakato wa visa.
Hatua ya 4: Kutolewa kwa Visa na Kuchukua Pasipoti
Baada ya maombi kukamilika, utapokea visa ya kielektroniki (e-visa) au visa iliyo wekwa kwenye pasipoti, kulingana na utaratibu unaotumika.
Hatua ya 5: Kuhifadhi Kibali kupitia Nusuk App
Jisajili kwenye Nusuk App, sajili taarifa za visa yako na uweke booking ya muda maalum kwa ajili ya kufanya Umrah na kutembelea Rawdah.
Tofauti kati ya Visa ya Umrah ya Ingizo Moja na Visa ya Mwaka Mmoja yenye Ingizo Nyingi
Nyaraka Zinazohitajika kwa Waombaji kutoka Tanzania
Pasipoti halali: Lazima iwe na uhalali wa angalau miezi 6.
Picha ya Pasipoti: Picha ya passport yenye background nyeupe.
Kadi/Cheti cha Chanjo: Cheti cha chanjo ya Meningococcal ACWY.
Nusuk Booking Reference (BRN): Namba ya booking ya hoteli iliyo idhinishwa na usafiri wa ndani ya Saudi Arabia.
Weka Nafasi Yako ya Visa ya Umrah kupitia City Squares
City Squares, iliyopo Upanga, Dar es Salaam, inatoa huduma kamili za usindikaji wa visa za Umrah.
Huduma zetu zinajumuisha:
Booking ya hoteli na usafiri wa Saudi Arabia kupitia huduma zilizo idhinishwa na kupata Nusuk BRNs.
Msaada katika kuwasilisha nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya mchakato wa visa.
Msaada wa haraka katika mchakato wa maombi na ufuatiliaji wa visa.
Ushauri na msaada kwa wasafiri binafsi, familia na vikundi vya wasafiri.
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp Connect with us on WhatsApp, au panga muda maalum wa kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu wetu wa huduma za safari na biashara.
Au wasiliana nasi hapa Connect with us here, Jaza fomu iliyo hapa chini au weka miadi ya ushauri wa mtu mmoja kwa mmoja (1-on-1 consultation).
Viungo Muhimu vya Huduma Zetu
Huduma za Usajili wa Kampuni Tanzania: : Company Formation Service
Huduma za Ubalozi wa Saudi Arabia: Saudi Embassy Services
Huduma za Ajira: : Employment Services
Huduma za Usafirishaji na Uondoaji wa Mizigo: Logistics Services
Rasilimali za Ziada
Huduma za Usajili wa Kampuni Tanzania: Launch your business with City Squares
Weka Miadi: Book a 1 on 1 Free Video Meeting with Our Expert Consultant
Kuhusu Sisi: Discover City Squares
Nakala Zetu: Explore All Articles
Usafirishaji wa Makontena hadi Bandari ya Dar es Salaam
Kampuni Bora za Usafirishaji kutoka Ghuba hadi Tanzania
Je, Usafirishaji hadi Tanzania Unagharimu Kiasi Gani
Kampuni Bora ya Usafirishaji Tanzania
Taratibu za Forodha nchini Tanzania
Machapisho ya Hivi Karibuni
Uko tayari kuanza mradi wako? Omba huduma yako na anza safari yako nasi!
Mtaalamu wa Kimataifa Mohammed bin Rashid bin Adwan